Rasmi Sasa Burna Boy Ampokonya Ufalme Diamond Platnumz


Rasmi Sasa Burna Boy Ampokonya Ufalme Diamond Platnumz

The Platnumz Voice, Naseeb Abdul, amevuliwa Taji la ufalme wa kuwa na idadi kubwa ya watazamaji wa jumla (viewes) katika mtandao wa YouTube kwa ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.
@diamondplatnumz ameishikilia namba moja kwa muda mrefu kabla ya The African Giant, @burnaboygram mwenye subscribers zaidi ya milioni 4, kupokea taji hilo la Ufalme, akiwa na watazamaji bilioni 2,247,168,799 tofauti ya watazamaji zaidi ya millioni 4 na Diamond mwenye watazamaji billioni 2,243,099,382 na subscribers karibu milioni 8.
Mwezi Juni 12, 2011. Bosi huyo wa WCB Wasafi na mfanyabiashara nchini, alijiunga rasmi na mtandao huo wa ku-stream muziki, na miaka saba baadae mwimbaji wa Nigeria, Ogulu, nae mwezi Januari 13,2018 alijiunga na YouTube.

Hii hapa orodha ya wasanii watano (5) wenye watazamaji wengi wa jumla YouTube, katika ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara

1.Burna Boy - Bil. 2.247
2.Diamond Platnumz - Bil. 2.243
3.Wizkid - Bil. 1.7
4.Fally Pupa - Bil. 1.5
5.Davido - Bil. 1.3

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad