Sababu ya TIMU ya Kitayosce (Tabora United) Kuingia na Wachezaji Nane Uwanjani Dhidi ya Azam FC Yatajwa



TIMU ya Kitayosce (Tabora United) ya Tabora imeingia na wachezaji pungufu uwanjani kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara (NBC PL) dhidi ya wenyeji Azam FC kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam sababu kubwa ikielezwa kuwa wachezaji wao wamekosa vibali.

Kitayosce (Tabora United) wameingia na wachezaji nane pekee akiwemo na golikipa kwenye mchezo huo wa kufungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya msimu uliopita kupanda daraja.

Vile vile, kwenye benchi lao la ufundi ameonekana mtu mmoja pekee. Azam FC wameingia uwanjani idadi ya wachezaji wote 11 wanaotakiwa kisheria na taratibu, kwenye dakika ya 3’ 9’ 13’, Kiungo Feisal Salim (Feitoto) amefunga Hat Trick, Prince Dube amefunga bao moja kwenye dakika ya 5’ na kufanya ubao kusomeka 4-0.

Afisa Habari wa Bodi ya Ligi, Karim Boimanda akizungumza na Azam TV wenye dhamana ya kuonyesha Ligi hiyo, amesema mchezo huo umelazimika kumalizwa na Mwamuzi baada ya Kitayosce (Tabora United) kushindwa kutimiza matakwa ya Kanuni namba 17, ibara ya 30 ya Ligi hiyo ambayo inaaeleza kuwa mchezo utaendelea endapo timu ina wachezaji wasiozidi 11 na wasiopungua saba.

“Waliingia na wachezaji saba (walikuwa nane) Kikanuni walikuwa sawa kabisa, lakini baada ya kuumia wachezaji wao wawili, Kanuni hiyo namba 17 ibara ya 31 inaeleza endapo wachezaji watakuwa pungufu chini ya saba, basi mchezo husika utavunjwa kutokana na upungufu wa wachezaji wa timu husika,” amesema Boimanda.

Boimanda amesema mabao ya Azam FC yanatambulika sanjari na Hat Trick ya Kiungo Feisal Salum (Feitoto) ambaye amefunga mabao matatu pekee yake huku Prince Dube akifunga bao moja na kufanya wenyeji kuondoka kifua mbele na jumla ya mabao 4-0.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad