Samia acharuka wananchi wanaojibu hawana nafasi wanapoitwa na Serikali

 

Samia acharuka wananchi wanaojibu hawana nafasi wanapoitwa na Serikali

Rais Samia Suluhu Hassan amechukizwa na baadhi ya wananchi waliovamia maeneo ya utafiti ambao wanaitwa kwa lengo la kuzungumza na Serikali wanajibu kuwa hawana nafasi.


Rais Samia ametoa kauli hiyo leo katika kilele cha maadhimisho ya Nanenane jijini Mbeya ambapo amesema anazitaka taasisi za utafiti kulinda maeneo yao ili kujua ni kina nani wamevamìa kwa kiasi gani maeneo hayo.


Amesema wananchi unajijua kabisa umeshafanya kosa, unaitwa na Serikali kuzungumza ili kufikia makubaliano mnajibu hamna nafasi.


“Hii maana yake nini, mnailazimisha Serikali kuchukua hatua zipi? Sasa naomba turudi kwenye meza pamoja,” amesema Rais Samia na kuongeza


“Kilimo bila utafiti hatuwezi kwenda vizuri tumefika hapa tunapojisifia kwa sababu ya utafiti na uzalishaji wa mbegu, sasa tukiachia maeneo haya yachukuliwe tunakwenda kudumaza shughuli za utafiti na uzalishaji wa mbegu


“Nikuombe Waziri kaa na Serikali ya mkoa wa Mbeya hapa lakini na maeneo mengine kulikovamiwa kaa na Serikali za huko za mikoa muangalie njia muafaka za kuwatoa wananchi hao waliovamia,” amesema

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad