Serikali Somalia yaomba radhi kwa kupeleka mkimbiaji 'anayekimbia taratibu' kwenye mbio za kimataifa






Waziri wa michezo wa Somalia ameomba radhi baada ya mshiriki mwanamke katika mbio za kimataifa za mita 100 kuonekana akikimbia taratibu kiasi kwamba watu wanahoji aliwezaje kuchaguliwa.

Katika mashindano ya michezo ya vyuo vikuu katika mji wa Chengdu nchini China, Nasra Abubakar Ali alitumia karibu sekunde 22 kumaliza mbio hizo - karibu mara mbili ya muda aliyoutumia mshindi.


Katika video ya tukio hilo, ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwanariadha huyo wa Somalia alionekana kukimbia kama sio mwanariadha, taratibu na kuonekana kama vichekesho.

Waziri wa Michezo Mohamed Barre Mohamud alitaja tukio hilo kuwa la aibu. "Kilichotokea leo haikuwa uwakilishi wa watu wa Somalia... tunaomba radhi kwa watu wa Somalia," alisema.

Inaelezwa kuwa ukweli wa kwamba hakuwa na uzoefu wa kushindana umewafanya baadhi ya Wasomali kushangaa kwa nini alichaguliwa.


Kama kilichofanyika ni kupata umaarufu na kujulikana inaelezwa kwenye mitandao kwamba, ameshinda sawa na medali ya dhahabu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad