Shaffih Dauda: Ya Mzize haikuwa Offside, ya Kibu ni penati halali

 

Shaffih Dauda: Ya Mzize haikuwa Offside, ya Kibu ni penati halali

Wakati lawama zikiendelea kushuka kwa waamuzi kushindwa kulimudu pambano la watani wa Jadi la Fainali ya Ngao ya Jamii 2023 iliyopigwa Mkoani Tanga.


Wengi wanaongelea tukio la Golikipa wa Simba Ally Salim kutoka katika eneo lake wakati wa upigaji wa Penati na kusema waamuzi walipaswa kuwa makini kwani ilipaswa penati zote zirudiwe.


Sasa Mchambuzi wa michezo kutoka Clouds FM, Shaffih Dauda yeye amekuja na mtazamo tofauti na yale wanayozungumza wengi.


Shaffih anasema;


“Hili la kipa kutoka kwenye mstari ni kwamba mechi ya Simba na Yanga lazima Mwamuzi atatafutiwa angle ya lawama , kwangu kulikuwa na matukio makubwa mawili penati ya Kibu na offside ya Mzize kama kungekuwa na teknolojia kulikuwa na nafasi ya Simba kupata penati na bao la Yanga kukubaliwa “

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad