Simba Unyama Mwingi Sana, Ubunifu wa Kuuza Kibegi na Jezi Zenye Majina ya Viongozi Mnadani Waingiza Mkwanja Huu


Simba Unyama Mwingi Sana, Ubunifu wa Kuuza Kibegi na Jezi Zenye Majina ya Viongozi Mnadani Waingiza Mkwanja Huu
Kibegi cha Simba

Kibegi kilichokuwa na jezi za Simba na kupelekwa juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Saleh Majapa katika Mnada uliofanyika katika ofisi za Azam TV.

Jezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan imeuzwa kwa Sh. 10,000,000 kwa Benki ya CRDB katika Mnada unaoendelea katika ofisi za Azam TV.

Jezi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Philip Mpango imeuzwa kwa Sh. 3,000,0000 kwa Sandland Omary ‘Sandland The Only One’

Jezi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Akson imeuzwa kwa Sh. 2,500,000 kwa Tawi la Simba Makini

Jezi ya Rais wa Heshima wa klabu, Mohamed Dewji 'Mo' @moodewji imeuzwa Sh. 2,000,000 na Duka la Vifaa la Michezo la Romario Sports

Jezi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi imeuzwa Tsh. 5,000,0000 kwa Hasa Clearing and Forwarding

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad