Simba Yaifunga Mtibwa Sugar 4-2 Ligi Kuu Bara

 

Simba Yaifunga Mtibwa Sugar 4-2  Ligi Kuu Bara

Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wameibuka na ushindi mzito wa bao 4-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.


Mchezo huo uliokuwa na kasi kwa timu zote mbili umechezwa kwenye Uwanja wa Manungu mkoani Morogoro ambapo Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata magoli ya kuongoza kupitia kwa Jean Baleke na Willy Onana kipindi cha kwanza.


Hata hivyo, Mtibwa walifanya come back ya maana ndani kipindi hichohicho cha kwanza na kufanikiwa kusawazisha. Lakini hata hivyo Fabrice Ngoma aliongeza goli la 3 na kuifanya Simba iende mapumziko ikiwa mbele kwa 3-2.


Kipindi cha pili kilianza kwa Mtibwa kufanya mashambulizi ya kasi lakini hata hivyo hawakufanikiwa kupata chochote na hatimaye Claotus Chama alifanikiwa kutupia msumali wa nne ambao ulisimama hadi mwisho wa mchezo.


Hadi mwisho, Simba ilimaliza kwa ushindi huo mzito wa kwanza katika Ligi ya NBC 2023-24.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad