Singida FG kukiwasha shirikisho Afrika leo




KLABU ya Singida Fountain Gate leo inaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Mchezo huo wa awali utafanyika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, Dar es Salaam.

“Leo tupo na maafande wa Zanzibar machalii wa mtaa wa mtoni kijichi pale Zanzibar leo moto inalia wawa,” imesema Sindiga FG kupitia mitandao yake ya kijamii.

Timu nyingine inayoshiriki michuano hiyo ni Azam ambayo imeondoka leo kwenda Ethiopia kuikabili Bahir Dar Kenema ya nchi hiyo Agosti 20.


Yanga na Simba zinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika huku Yanga ikiikaribisha ASAS Djibouti kwenye uwanja wa Azam Complex Agosti 20.

KOMBE LA SHIRIKISHO
Art/Solar7 vs Horseed
Gaborone United vs Assm Elgeco Plus

LIGI YA MABINGWA
KMKM vs Saint George SC
ASKO vs FAR Rabat
SC Constantine vs Etoile du Sahel

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad