Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema haijahusika kwa namna yoyote na ufungaji wa The Cask Bar & Grill ya iliyopo Jijini Mwanza.
TRA imesema “Tunaomba Wahusika na Umma wawasiliane na Mamlaka husika juu ya jambo hilo”
Itakumbukwa jana Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Kiomono Kibamba alitangaza kufungia The Cask kwa tuhuma za ukwepaji kodi kwa kipindi cha miaka miwili ambapo alinukuliwa akisema Bar hiyo imekwepa kodi ya Serikali na kuendesha biashara zaidi ya moja eneo hilohilo.
Kiomono alinukuliwa akisema pia Bar hiyo imekiuka masharti ya leseni za biashara, pia imekosa leseni za biashara za vileo kwa miaka miwili na shida nyingine za kimapato.