Unaambiwa Yanga Hapakaliki Kuridhi Nafasi ya Fiston Mayele, Kennedy Musonda Apigishwa Kwata la Hatari

Unaambiwa Yanga Hapakaliki Kuridhi Nafasi ya Fiston Mayele, Kennedy Musonda Apigishwa Kwata la Hatari


MIGUEL Gamondi Kocha Mkuu wa Yanga anaendelea kumsuka upya mrithi wa mikoba ya, Fiston Mayele ambaye ni Kennedy Musonda.

Mayele hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kupata dili katika kikosi cha Pyramids ya Misri huku akibainisha kuwa anaondoka sehemu aliyopokelewa vizuri.

Akiwa Yanga, Mayele alibeba Tuzo ya ufungaji bora msimu uliopita, mchezaji bora wa msimu ‘MVP’, bao bora na alikuwa ndani ya kikosi bora cha msimu hivi vinadhihirisha uimara wake wakati akiwa Jangwani.

Kuondoka kwa Mayele kumempa nafasi Musonda kuwa chaguo la kwanza upande wa washambuliaji huku akiongezwa nyota mwingine, Hafiz Konkoni raia wa Ghana.

Katika programu ambazo Musonda anaendelea nazo kambini AVIC Town ni pamoja na mazoezi maalumu ya kufunga pamoja na kumwaga krosi kwa wachezaji wenzake.

“Musonda anaendelea na mazoezi chini ya Gamondi akishirikiana na wachezaji wengine ambapo amekuwa akipewa jukumu la kufunga pamoja na kutengeneza pasi za mabao.

“Mwalimu amekuwa akimpa mipira mingi huku akimtaka afunge mabao zaidi ya matano langoni hilo linazidi kumuimarisha, hivyo atakuwa katika ubora kwenye mashindano yote,” kilisema chanzo.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe aliliambia soka la bongo kuwa Musonda ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kutokana na rekodi.

“Musonda ana rekodi nzuri na hilo lipo wazi kwani anatengeneza nafasi na anafunga hivyo mashabiki wa Yanga ni muhimu kuwa na imani na kutambua kwamba tuna mtu wa kazi,” alisema Kamwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad