Wakili: Mwanamke Ukimpa Talaka Unatakiwa Umhudumie Mpaka Aolewe

Wakili: Mwanamke Ukimpa Talaka Unatakiwa Umhudumie Mpaka Aolewe

Wakili: Mwanamke Ukimpa Talaka Unatakiwa Umhudumie Mpaka Aolewe 

Uliwahi kufahamu kwamba, mwanamke aliyeachika tena kwa talaka ana haki zake za msingi ambazo anatakiwa kuzipata kutoka kwa aliyekuwa mumewe (yaani mtalaka wake) ikiwemo kumtunza na kumhudumia?


Sasa huyu hapa Wakili Frednand Makole ambaye anatusanua Sheria ya Ndoa ya Tanzania inasemaje kuhusu mwanamke aliyepewa talaka na mumewe.


“Ukiangalia kifungu cha 120 ni ‘very interesting’, kinasema hata baada ya kuachana, hata baada ya talaka, mwanaume anatakiwa aendelee kumhudumia mwanamke (aliyekuwa mkewe/mtalaka wake) mpaka pale atakapoolewa tena.


“Kifungu hiki watu hawakisemi kwa sababu presumption ni kwamba mkiachana kila mtu anachukua la kwake lakini sheria ipo inaitwa ‘Right to maintenance on cease to marriage’ hii ni haki ya kila mwanamke aliyeachika kupewa huduma na huyo mtalaka wake.


“Sasa kivumbi ni pale ambapo mwanamke huyu haolewi, au akikosa wa kumuoa. Hii ni sawa na sheria ya ajira imempa faida zaidi mwajiri, hata hii imempa faida zaidi mwanamke," amesema Wakili Frednand Makole.


Nini maoni yako?


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad