Watu 10 wamefariki dunia hii leo Agosti 18, 2023, Ajali ya Kirikuu na Gari la Polisi


Watu 10 wamefariki dunia hii leo Agosti 18, 2023, katika ajali iliyohusisha gari dogo la mizigo (kirikuu) lenye namba T 292 DEU na gari la Polisi PT.4081 Ashok Leyland lililokuwa likiendeshwa na Ex.G.8813 CPL.Denis amnbaye naye amefariki.

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Dachi Kona Barabara ya Sanya Juu mkoani Kilimanjaro umbali wa kilomita 50 kutoka mjini Moshi.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema chanzo cha ajali hiyo ni kupasuka tairi la kirikuu kisha kuhama barabara na ndipo magari hayo yalipokutana uso kwa uso.

Hospitali ya Kibong'oto imethibitisha kupokea miili ya watu 10 na miongoni mwao saba ni wanawake ambao walikuwa kwenye kirikuu. @daupizo_

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad