Yanga Kuvunja Benki ili Kumrudisha Simon Msuva Nyumbani, Kocha Amtaka Kwa Udi na Uvumba

Yanga Kuvunja Benki ili Kumrudisha Simon Msuva Nyumbani, Kocha  Amtaka Kwa Udi na Uvumba

Kuna hesabu ngumu mabosi wa Yanga wanazipiga juu ya kukiboresha kikosi chao hasa juu ya kuiongezea makali safu yao ya ushambuliaji na kuna mastraika watatu wanaumiza vichwa vya vigogo wa timu hiyo huku jina la Simon Msuva likirejea mezani.


Yanga inafikiria kurudi sokoni baada ya kununua mtu wa haraka wa kuwafungia mabao baada ya Kocha Miguel Gamondi kugundua kwamba washambuliaji wanne alionao wanahitaji muda zaidi kumpa anachotaka.


Yanga haraka wakaanza hesabu za kusaka mshambuliaji mpya atakayekuja kusaidiana na hao wanne huku mezani kwao kukiwa na washambuliaji Mkongomani Makabi Lilepo wa Al Hilal, Simon Msuva na George Mpole.


Ugumu wa usajili wa Lilepo ni kwamba, utailazimisha Yanga kuondoa jina moja la mchezaji wa kigeni kati ya nyota 12 walipo ikiwa idadi kamili ya kikanuni kwa wageni hao.


Hesabu za pili kwa Yanga ni kumsaka mshambuliaji mzawa na tayari walishamvutia waya George Mpole ambaye ni mali ya FC Lupopo ya DR Congo akawaambia yuko freshi ni wao tu.


Lakini yote kwa yote karata kubwa ya Yanga na inayowaumiza kichwa zaidi ni Simon Msuva. Wanapiga hesabu za jinsi gani ya kumshawishi kiutu uzima arudi nyumbani.


Yanga inajua msimamo wa Msuva anayetaka kuendelea kucheza nje akiwahi kuliambia Mwanaspoti kuwa anaweza kuja kurejea klabu yake hiyo iliyomuuza nje kwa mara ya kwanza lakini sio kwasasa.



Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi ameliambia Mwanaspoti kuwa;


“Simba pekee ndio wanaweza kusajili sasa bila kikwazo, na sababu zao ni mbili kwanza ni kutokana na hatua yao ya kuanzia hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na sababu ya pili ni hiyo ya ushiriki wao wa Super Cup,”


“Klabu zingine zinaweza kusajili lakini hapo wanaweza kukutana na malipo ya adhabu lakini kikubwa hapa ni kama hiyo klabu itatoa sababu nzito ambayo CAF itawaridhisha na kuwapa hiyo nafasi.


“Unajua hizo klabu tatu za Yanga, Singida na Azam wao wanacheza wiki hii na ndio maana nasema lazima kuwe na sababu kubwa itakayowapa mashiko CAF na kuwapa hiyo nafasi ya kusajili,” amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad