Yanga Watangaza Siku ya Kurudi Mchezaji Skudu Makudubela

 

Yanga Watangaza Siku ya Kurudi Mchezaji Skudu Makudubela

Meneja Habari na Mawasiliano wa Yanga, Alli Kamwe akizungumza leo na waandisi wa habari amesema kesho siku ya Ijumaa Mahlatse Makudubela 'Skudu' atarejea nchini akitokea nchini kwao Afrika Kusini alipokwenda kushughulikia hati yake ya kusafiria (passport) ambayo imejaa.


"Skudu kweli alisafiri kwenda Afrika Kusini na kesho Ijumaa atarejea nchini Kocha Gamondi akitaka kumtumia Jumamosi ni maamuzi yake , amepona kabisa na tuliwaaambia amekwenda kushugulikia passport yake ya kusafiria"


Skudu alishindwa kuendelea na mchezo katika Nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Azam, baada ya kuchezewa rafu dakika ya saba na kiungo wa Azam, James Akaminko.


Na Yanga iliichapa Azam 2-0 mabao yalifungwa na Aziz KI na Clement Mzize ambayo yamefungwa katika dakika 10 za mwisho za mchezo huo.


Skudu ameweka rekodi ndani ya Yanga ya kuwa mchezaji wa kwanza raia wa Afrika Kusini kuwatumikia mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC na Kombe la Shirikisho la Azam.


Mbali na Marumo staa huyo pia amewahi kuzichezea timu za Afrika Kusini, Chippa United na Orlando Pirates kwa mafanikio makubwa, anatajwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye uzoefu sana kwenye Ligi Kuu Afrika Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad