Zitto Kabwe Abadili Kamati ya Wasemaji ACT Wazalendo

 


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefanya mabadiliko ya Kamati ya wasemaji wa kisekta ya chama hicho leo Agosti 6, 2023.


Kupitia taarifa iliyotolewa leo na ofisa habari wa Ofisi ya Baraza Kivuli, Abdallah Khamis, Zitto kwa kushirikiana na Waziri Mkuu kivuli Doroty Semu amefanya mabadiliko hayo ikiwa ni kuongeza ufanisi katika shughuli za Baraza Kivuli na kuongeza nguvu ya chama katika kupendekeza sera mbadala.


“Katika mabadiliko haya uwiano wa kijinsia umeimarika. Pamoja na Waziri Mkuu Kivuli ambaye ni mwanamke, Kiongozi wa chama ameteua jumla ya wasemaji wanawake (Mawaziri Vivuli) 14 kati ya wasemaji wote 25, sawa asilimia 54 ya wasemaji wote,” imeeleza taarifa hiyo.


Mabadiliko hayo yanahusisha Ofisi ya Rais Mipango, Uwekezaji na Hifadhi ya Jamii ambapo Emmanuel Mvula amekuwa Msemaji na Shangwe Ayo kuwa Naibu wake.


Katika Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Pavu Juma ameteuliwa kuwa msemaji pamoja na Bahati Chirwa kuwa Naibu Msemaji.


Vilevile Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini, Kulthum Mchuchuli ameteuliwa kuwa Msemaji na Hussein Ruhava kuwa Naibu Nsemaji Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini pia Aika Peter naibu Msemaji Tawala za Mikoa.


Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano, Mazingira na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi, John Mbozu amekuwa Msemaji na Seif Suleiman kuwa Naibu.


Pia, Ally Alberto amekuwa msemaji ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu, Estazia Kangwa amekuwa naibu msemaji Uratibu pia msemaji mkuu wa kamati, vilevile, Salma Mbarouk ni naibu msemaji wa Sera na Bunge.


Katika sekta ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ameteuliwa Fatma Fereji kuwa Msemaji na Stanley Mbembati kuwa Naibu.


Bonifasia Mapunda ameteuliwa kuwa Msemaji Sekta ya Mambo ya Ndani ya Nchi pamoja na naibu wake Khadija Anwar.


Katika Sekta ya Fedha ameteuliwa Esther Thomas kuwa Msemaji na Dk Mohamed Suleiman kuwa Naibu wake.


Dk Nasra Omar ameteuliwa kuwa msemaji sekta ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Muhidin Mkwera kuwa naibu.


Katika Sekta ya Afya, Dk Elizabeth Sanga ameteuliwa kuwa Msemaji na Ruqayya Nassir Naibu Msemaji.


Msemaji sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni Riziki Ngwali pamoja na Makalanga Ntebe naibu wake.


Isihaka Mchinjita ameteuliwa kuwa Msemaji Sekta ya Nishati na Juma Hamad kuwa Naibu wake.


Rasilimali Madini na Migodi, Edgar Mkosamali ni msemaji na Raya Khamis, Naibu Msemaji.


Mwanaisha Mndeme, msemaji sekta ya Maji na Marijani Ndandavale kawa naibu msemaji.


Sekta ya kilimo, Umwagiliaji na Maendeleo ya Ushirika, Mtutura Mtutura, msemaji na Said Bakema kuwa Naibu.


Katika sekta ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Kiza Mayeye kawa Msemaji na Naibu wake ni Vitali Maembe.


Philbert Macheyeki ameteuliwa kuwa Msemaji Mekta ya Habari, Mawasiliano na TEHAMA na Selemani Misango kuwa Naibu.


Viwanda na Biashara ameteuliwa Halima Nabalang'anya kuwa Msemaji na Julius Massabo kuwa Naibu Msemaji.


Sekta ya Maliasili na Utalii ameteuliwa Juliana Mwakang'wali kuwa Msemaji na Anthony Ishika kuwa Naibu.


Katiba na Sheria ameteuliwa Mbarala Maharagande kuwa Msemaji na Christina Mkundi kuwa Naibu.


Webiro Wasira ameteuliwa kuwa msemaji sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo na Monalisa Ndala ni Naibu.


Miundombinu na Uchukuzi ameteuliwa Mhandisi Mohamed Mtambo kuwa msemaji na Mhandisi Fidel Christopher kuwa naibu.


Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ameteuliwa Janeth Rithe kuwa Msemaji na Malaika Millinga kuwa Naibu msemaji.


Sekta ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameteuliwa Mhandisi Ndolezi Ndolezi kuwa msemaji na Dahlia Hassan kuwa Naibu.


Vijana, Kazi na Ajira ameteuliwa Abdul Nondo kuwa msemaji na Felix Kamugisha kuwa Naibu.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad