Aggy Baby Amuonya Harmonize Kumtaka Kimapenzi

 

Aggy Baby Amuonya Harmonize Kumtaka Kimapenzi

Msanii wa Bongo Fleva na mjasiriamali, Agness Suleiman maarufu kama Aggy Baby amemuonya vikali msanii Harmonize na kumtaka aache kumtumia meseji DM, wala kumtafuta na kumtumia meseji.


Aggy amemwambia bosi huyo wa Lebo ya Konde Ganga kuwa, asione kila mwanamke ambaye anamuonekano mzuri ni malaya na kumtaka kimapenzi, badala yake atunze heshima yake kabla hajamlipua pakubwa zaidi.


"Nampa onyo Harmonize, asione kila mwanamke mwenye shepu ni malay* wa kudeti naye, aache kunitafuta na kunifatilia, aache kuni-DM na kunitumia meseji.


"Siyo wanawake wote wenye shepu anaweza kuwachezea, wengine tunajiheshimu na tuna maisha yetu lakini pia tuna kazi zetu," amesems Aggy Baby.


Hata hivyo Aggy alionyesha meseji hizo ambapo Harmonize alikuwa anamchombeza kwa maneno ya kimahaba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad