Ahmed Ally "Yanga si Kipimo Sahihi Kwetu, Hatuwezi Kucheza nao"

Ahmed Ally "Yanga si Kipimo Sahihi Kwetu, Hatuwezi Kucheza nao"

 Ahmed Ally "Yanga si Kipimo Sahihi Kwetu, Hatuwezi Kucheza nao"

Ofisa Habari wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema klabu yao haiweze kucheza na wapinzani wao, Yanga Sc mechi ya kirafiki kujiandaa na mechi dhidi ya Power Dynamos ya Zambia.


Ahmed Ally akijibu swali la mwandishi ambaye aliuliza kwa nini Simba wasiombe kucheza na Yanga mechi ya kirafiki kuliko kuhangaika kutafuta mechi za ushindani za ndani na nje.


“Hatuwezi kucheza mchezo wa kirafiki na Yanga kwa sababu haiwezi kutupatia kipimo halisi tunachokihitaji, level zetu na wao ni tofauti sana, sisi tunawaza kucheza Nusu Fainali wao wanawaza hatua ya makundi.


"Tukicheza hii mechi inakuwa kama mtu tall kucheza na kajitu kadogo, tunakuwa kama tunajidanganya wenyewe, ili tupate taste halisi lazima tutafute timu ambayo inafanana kariba na Klabu ya Simba.


"Power Dynamos msiwachukulie poapoa ukienda kichwa kichwa anakuadhibu. Kwa hiyo lazima tutafute mechi za ushindani, timu nzuri zenye manufaa na Simba SC.


"Azam ni mshindani nzuri ila ukimpelekea moto sawasawa anavunja mechi, kwa hiyo huwezi kupata kile unachokitaka.


"Katika kipindi chote cha kambi tunatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki. Tunasubiri uthibitisho wa timu ambazo tutacheza nazo, moja ya nje na nyingine ya ndani. Lengo letu kama Simba ni tupate mechi ngumu, mechi ya kiushindani," amesema Ahmed Ally.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad