Alex Ngereza: GSM anainyonya Yanga



Mchambuzi wa masuala ya soka nchini kupitia runinga ya TV3, Alex Ngereza amedai kuwa mdhamini wa Klabu ya Yanga, Gahalib Said Mohamed (GSM) anainyonya klabu hiyo.

Kupitia mitandao yake ya kijamii, Ngereza ameandika;

Kama jezi moja inauzwa kwa shilingi Elfu 40 sio mbaya kwa Yanga kupata hata 20 kwenye kila jezi moja lakini kitendo cha jezi inauzwa shiling Elfu 40 na Yanga wanapata shiling Elfu moja na mia tatu au mia sita inakuwa sio sawa kabisa.

Bora wangeingia mkataba kama Simba walivyofanya wao wanachukua Billion zao mbili kwa mwaka full stop hawana tena muda wa kuangalia kwamba zimeuzwa au hazijauzwa na wao hawapati hasara kama Simba.


"Yanga inaweza kujiendesha bila GSM kama fedha za wanachama zinaweza kuipeleka timu fainali ya CAF Confideration kwa fedha za wanachama tu bila kuchukua fedha nyingine kutoka sehemu nyingine yoyote.

"Kama wanachama wanaweza kutoa zaidi ya Billion moja kwa mwaka mmoja manake ukitengeneza mfumo mzuri timu inaweza kupata hata Billion tano kwa mwaka kupitia wananchama.

"Kitu ambacho kitasaidia kujitoa kuwa tegemezi kwa watu kama GSM ambao wanapata fedha nyingi kupitia Yanga bila mashabiki na wanachama kujua. Kwa kifupi kuna namna GSM anainyonya Yanga," amesema Ngereza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad