Hii ni baada ya Shirikisho la Kimataifa la kutunza Takwimu na Historia za mpira Duniani ‘IFFHS’ kutoa Orodha ya Timu 10 bora barani Afrika kwa mwaka mzima (kuanzia Septemba 1, 2023- Agosti 31, 2023).
Yanga imeshika nafasi ya 3 nyuma ya Al-Ahly na Wydad Casablanca.
Duniani Yanga ipo nafasi ya 63, juu ya Chelsea (72).
Ni afajiri ya kuamkia leo ambapo mashabiki na wanachama wa Yanga sambamba na viongozi mbalimbali wakielekea nchini Rwanda kwenye mchezo na Al-Merrekh.
“Ukienda kwenye website ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), linatambua na limetunza rekodi zinazoteolewa na shirikisho lile, kwa hiyo hutakiwi kubishana na mimi, bishana na takwimu. Ukitaka kutoa povu kabishane na takwimu usibishane na mimi.
“Wale ndiyo ndiyo wamekaa, wamepitia wametoa zile alama kwamba Yanga sasa hivi tuko nafasi ya tatu. Na sisi Yanga tumeumia, tunataka tuwe nafasi ya kwanza na sio nafasi ya tatu. Kwa hiyo tunaongeza juhudi ili wakati ujao tuwe namba moja.
“Kama pale 10 Bora haupo, waambie wenye shirikisho washushe 50 bora au 100 bora huko, mkutane huko chini. Pale ni kwa ajili ya watu 10 tu tunaojitambua barani Afrika, tunajitambua,” amesema Ally Kamwe.