Beki Henock Inonga Atibua Mipango Simba SC




Beki wa Simba SC, Henock Inonga ametoka hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye mchezo wa juzi Alhamis (Septemba 21) huku kocha wake akitikisa kichwa na akisema muda ambao wanaweza kumkosa.

Inonga aliumia wakati Simba SC ikiifunga Coastal Union ya Tanga kwa mabao 3-0 ikiwa ni mechi ya Ligi Kuu Bara, aliumia katika dakika ya 20 kipindi cha kwanza na kuwahishwa hospitalini kushonwa jeraha hilo la mguuni baada ya kukanyagwa na Haji Ugando. Kilinda ugoko cha Inonga kilivunjika.

Kocha wa Simba SC, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ mwenye umri wa miaka 63 amesema kuumia kwa beki huyo kunatibua hesabu zake ambapo taarifa ya awali ya daktari wa timu ni kwamba ameshonwa nyuzi zisizopungua 12 na wanaweza kumkosa kwa siku kati ya 15-20.

Hata hivyo, daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo amesema bado wanasubiri ripoti kamili ya vipimo vingine ili waweze kutoa ripoti ya ujumla baadae mwishoni mwa juma hili.


Tunasubiri ripoti kamili ya vipimo vingine vya mguu wake na tutakapovipata tutatoa taarifa kamili ya muda gani atakuwa nje au utatumika kupona kwake,” amesema Kagabo..

Kwa upande wa Robertinho amesema; “Ni habari mbaya sana kwetu hasa wakati huu tunatafuta muunganiko wa timu yetu, tupo kwenye wakati wa kuiunganisha timu na mchezaji na beki bora Afrika ameumia vibaya.

“Kwa haraka haraka nadhani tunaweza kumkosa kwa siku 15 au 20, kile ni Kidonda kikubwa kilichohusisha ushonaji wa nyuzi kama 12 au zaidi, itategemea atakuwa na uponaji wa haraka kwa namna ipi, tunamuombea sana apone haraka” ameongeza.


Pia Robertinho amesema tukio lile liliwaumiza wachezaji wake kwa mshtuko kuwafanya kushindwa kujituma uwanjani mara baada ya kuona jeraha lake.

“Kuna mchezaji aliniomba nimtoe, lakini nilikataa ilihitaji kuwajenga kisaikolojia, wenzake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad