Kupitia akaunti rasmi ya Instahram ya bondia Hassan Mwakinyo (hassanmwakinyojr) ameandika;
"Binafsi, napenda sana Kushukuru Mwenyezi Mungu kwa uzima na afya nilionayo leo, pia niwashukuru sana washabiki zangu kwa kujitokeza kwa nguvu kuonyesha shauku ya kunisapoti, nawashukuru sana Azam TV kwa kuendelea kutoa nafasi. Kwetu kama wachezaji wa ndani naomba niweke hisia zangu wazi kwa mashabiki ya kuwa kesho sitaweza kupanda ulingoni kutokana na uongo na udanganyifu wa mapromota, binafsi sina tatizo na mtu ila pia naheshimu sana kazi yangu na siko tayari kuona watu wana nijaribu au kutaka kuharibu jina langu,"
Mwakinyo ametoa siku ya leo kutatuliwa changamoto aliyodai inakwamisha pambano hilo ili aweze kupigana kesho na bondia Julius Indongo wa Namibia baada ya kubadilishiwa mpinzani Rayton Okwiri