BREAKING: Nay wa Mitego Aitwa Central Polisi Kisa Wimbo Afunguka Haya



Rapper Nay wa Mitego amewasili katika kituo cha Polisi Kati ( Police Central) Jijini Dar es salaam kuitikia wito kuhusu wimbo wake wa ‘Amkeni’ ambao hivi karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitangaza kuufungia kuchezwa katika vituo vyote vya Radio na Televisheni.

Nay ambaye amewasili akiwa na Mwanasheria wake Jebra Kambole amenukuliwa akisema “Ukiwa sauti ya Watu kuja sehemu kama hii ni kawaida, mimi ni sauti ya Watu acha nikawasikilize nitakuwa na cha kuongea lakini kwa sasa sina, nimeambiwa tu ni wimbo wangu wa ‘amkeni’ kwahiyo nataka nikajue umefanya nini, kuna tatizo gani”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad