Chama Atoa Kauli Nzito Kuelekea Mchezo Dhidi ya Power Dynamos

Chama Atoa Kauli Nzito Kuelekea Mchezo Dhidi ya Power Dynamos


Kiungo mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, amesema anawafahamu Power Dynamos ni wazuri lakini Simba ni timu kubwa hivyo lazima waoneshe ukubwa wao.


Chama ametoa kauli hiyo jana Septemba 13, 2023 mara baada ya kukamilika kwa mazoezi yao ya mwisho kabla ya kusafiri kuwafata Power Dynamos nchini Zambia hii leo Septemba 14, 2023.


"Tumeshacheza nao kama mara mbili kwenye Simba Day, wanaongezeka ubora siku hadi siku lakini sisi ni Simba, ni timu kubwa lazima tukaoneshe ukubwa wetu. Tuna malengo makubwa kwenye haya mashindano hivyo wachezaji tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo mazuri kutimiza malengo yetu na ya klabu," alisema Chama.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad