Dereva Bodaboda Afariki Baada ya Kugongwa na Basi la Mwendokasi



DEREVA bodaboda leo Jumanne Septemba 12, 2023 asubuhi amefariki baada ya kugongwa na Basi la mwendokasi katika Makutano ya Mataa ya Lumumba na Barabara ya Morogoro jijini Dar es Salaam

Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam ambao watatoa taarifa kamili ya tukio hili hapo baadaye, wamethibitisha kifo cha Dereva huyo ambaye imeelezwa kuwa aliingia kwenye barabara hiyo maalum ya Mabasi hayo.

Kutokana na ajali hiyo baadhi ya gari yamelazimika kutafuta njia mbadala kuendelea na safari kutokana na ajali hiyo kufunga njia halisi ya mwendokasi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad