Diamond Afunguka Mazito Anayoyapitia, Awataja Freemason




Diamond afunguka mazito anayoyapitia, awataja Freemason
Supastaa wa muziki nchini ambaye pia ni mfanyabiashara, Naseeb Abdul Juma Issaack, maarufu kama Diamond Platnumz kupitia kwenye akaunti yake amefunguka kuhusu changamoto anazopitia hasa kuzushiwa baadhi ya mambo na kutukanwa vikali mitandaoni.

Kupitia ukurasa wake wa Insta Story yake, Diamond ambaye ni CEO wa Wasafi Media na Lebo ya muziki ya WCB amepost picha iliyomuonesha akiwa amesinzia kwenye gari kisha kuandika maneno haya;

"Mimi nimekuwa mtu wa kupambana kila siku, napanda mandege kila siku, nalala wa mwisho, naamka wa kwanza, nakesha studio, sipatagi muda wa kupumzika lakini naumia kuona Watanzania wenzangu ndo wanaongoza kwa kutengeneza vitu vya kunidharirisha.

"Mara niko Freemason na mengine mengi, mimi ndo nimekuwa mtu wa kuongelewa mabaya mitandaoni kila siku. Mazuri yangu hayaongelewagi, kiukweli nayachukia sana maisha yangu.


"Ningekuwa nafatiza kila kinachoongelewa na watu kila siku ningekuwa nimeacha mziki toka zamani," amefunguka msanii Diamond Platnumz.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad