Dotto Biteko afunguka uteuzi wa Rais Samia




NAIBU Waziri Mkuu, Dotto Biteko, amesema Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa jukumu kubwa baada ya kumteua kushika wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Biteko ametoa kauli hiyo leo tarehe 6 Septemba 2023, jijini Dodoma, akizungumza katika mkutano wa maafisa ustawi wa jamii.

“Nimshukuru Rais Samia kwa kuniona miongoni mwa wengi kuwa nina uwezo wa kumsaidia nafasi hii, katika hatua ya mwanzoni si busara sana kuahidi mbingu lakini nataka niseme kwa moyo wa dhati nimeupokea uteuzi huu nikiwa na wajibu mkubwa mbele yangu, nikiwa na kazi kubwa mbele yangu,” amesema Biteko na kuongeza:

“Lakini kwa sababu Rais amenipa kazi hii, jambo ambalo namuomba Mungu ni kunipa bega la kubeba majukumu haya. Lakini katika jambo ambalo sitafanya kosa ni kukosea ili aliyenitumia asije akakwazika kesho akateua mwingine.”


Biteko aliyekuwa Waziri wa Madini, aliteuliwa na Rais Samia kuwa Naibu Waziri Mkuu, mwishoni mwa Agosti mwaka huu, pamoja na kuhamishiwa katika Wizara ya Nishati.




Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad