Eng Hersi "Mchezaji Akicheza Chini ya Kiwango Yanga Anafurushwa"


Mchezaji akicheza chini ya kiwango Yanga anafurushwa


Rais wa Yanga SC, Injinia Hersi Said ameweka wazi kuwa hawatamvumilia mchezaji yeyote atakayecheza chini ya kiwango.


Hersi ametoa kauli hiyo akiwa nchini Rwanda timu yake ikijiandaa kukipiga na Al Merrekh.


"Wanachama na mashabiki mmeshafanya kazi yenu, sisi viongozi tunamalizia kazi yetu mchana kabla ya mechi, kuna kikao huwa kinafanyika kabla ya mechi, nitakimaliza hicho. Saa 9 jukumu litakuwa ni la wachezaji na sisi tutawadai wafanye kazi kweli hakuna masihara.


Kama kuna mchezaji atacheza kwa kiwango ambacho hakitamrishisha mwanayanga Januari pako wazi hatucheki na mtu. Tupo hapa kuhakikisha timu inapata matokeo na ndio kitu ambacho wanachama mmetutuma sisi viongozi," alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad