Kiungo wa zamani wa klabu za Juventus na Barcelona, Arturo Vidal, amemkosoa kocha wa Manchester United, Erik ten Hag kwa kumuondosha Cristiano Ronaldo, ndani ya klabu hiyo.
Kwenye mahojiano yaliyofanyika kwenye mtandao wa Twich, Vidal alionesha kutoelewa uamuzi wa Kocha Erik Ten Hag, kumuondosa Ronaldo, licha ya mshindi huyo wa Ballon d’Or mara tano kuonesha kiwango bora. Kwenye mahojiano hayo, Vidal alisema kuwa.
"Yule kocha aliingia United vibaya. Hivi unaanzaje kumpunguza Cristiano Ronaldo? Ndivyo walivyo hawa jamaa. Ronaldo alikuwa mfungaji wake bora, na akamtoa kikosini. Hawa watu wenye vipara wanashida sana".