Faustine Ndugulile "Uchaguzi wa Mwaka 2020 Ulikuwa Mgumu Baada ya Kuletewa Paul Makonda"


Niseme Tu kwamba uchaguzi wowote si uchaguzi mwepesi lakini Sisi kama wanasiasa mara nyingi tunafanya tathimini zako unaangalia endapo utagombea mapokeo ya wananchi yatakuwaje?

Mwaka 2020 uchaguzi ulikuwa mgumu (ulikuwa na ugumu wake) ikiwemo mazingira ambayo yalitokea matokeo ya uchaguzi Mkuu lakini pia na aina ya wagombea ambao tulikuwa tunakwenda kushindana nao. Kama utakumbuka 2020 nilikuwa Naibu Waziri wa Afya lakini nilitenguliwa mwezi Mmoja kabla ya Bunge kuvunjwa na Miezi miwili kabla ya kuelekea uchaguzi Mkuu. Ilileta changamoto kidogo.

Lakini pia nilikuwa nashindana na aliyekuwa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda nayo pia ilikuwa na changamoto zake kwa sababu wakati tulipokuwa tunaelekea kwenye michakato ile alikuwa akivaa kofia zote mbili za ukuu wa Mkoa na Mgombea nafasi ya ubunge. Ilileta changamoto.

Sambamba na hilo siku Mbili kabla ya uchaguzi nilimpotezea Mzee wangu (Baba Yangu). Nilipitia mapito magumu. Nawashukuru Sana wananchi wa Kigamboni Imani yao ilikuwa kubwa Sana kwangu" Dkt Faustine Ndugulile @Faustine_ndugulile, Mbunge wa Jimbo la Kigamboni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad