FID Q Afunguka Sakata la Rich Mavoko Kuonekana Akiimba Kwenye Madhingira Yaliyoshtua Wengi


Rapa Fid Q (@therealfidq) ametoka hadharani na kutolea ufafanuzi kipande cha video ambacho kinamuonesha Msanii Rich Mavoko akitumbuiza kwenye mazingira ambayo mashabiki wengi waliingiwa na maswali na kuanza kuhoji inakuwaje Mavoko anatumbuiza kwenye eneo la wazi kama hilo na lenye vumbi?

Kupitia mtandao wa X/Twitter, Fid Q amefafanua kwamba, Mavoko alipata show 10 toka kwa watu wa nyimbo za ASILI wa upande ule wa kanda ya ziwa, show zote zimeenda poa kabisa kimuitikio na kimaokoto kwa ujumla.

Kwenye andiko lake anasema, anafikiri kilichowashtua wengi ni ukubwa wa Jukwaa (😁), ambapo amefafanua kwamba, Jukwaa ilibidi liachiwe nafasi kubwa kwa maana kuna watumbuizaji wengine wa NGOMA ZA ASILI hucheza na CHATU au hata VINYOKA VIDOGO VIDOGO, so kwasababu za kiusalama mashabiki hushauriwa kuuzingatia umbali. Fid Q alisema, Yote ya yote @richmavoko ni mzima wa AFYA na amecheka sana baada ya kugundua anatrend huko Twitter, na zaidi Mavoko ametusisitiza tuendelee kumkumbuka kwenye maombi na sala ili maokoto yawe mengi zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad