Fid Q Aibuka na ishu ya Rich Mavoko Kuonekana Akipiga Show vijijini

Fid Q Aibuka na ishu ya Rich Mavoko Kuonekana Akipiga Show vijijini


Msanii wa Hip Hop Bongo, Fid Q amefunguka baada ya Rich Mavoko kuonekana akiwa anafanya show mchana bila ya jukwaa.


Chini ni kile alichoandika Fid Q katika mtandao wa X.


"Mitandao itabaki kuwa undefeated. Lakini ukweli ni kwamba Mavoko alipata show 10 toka kwa watu wa nyimbo za ASILI wa upande ule wa kanda ya ziwa. Show zote zimeenda poa kabisa kimuitikio na kimaokoto kwa ujumla, ninafikiri kilichowastua wengi ni ukubwa wa jukwaa


"Jukwaa ilibidi liachiwe nafasi kubwa kwa maana kuna watumbuizaji wengine wa NGOMA ZA ASILI hucheza na CHATU au hata VINYOKA VIDOGO VIDOGO.. so kwasababu za kiusalama mashabiki hushauriwa kuuzingatia umbali.


"Yote na Yote: ni mzima wa AFYA na amecheka sana baada ya kugundua anatrend huku, zaidi ametusisitiza tuendelee kumkumbuka kwenye maombi na sala ili maokoto yawe mengi zaidi."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad