FULL STORY: Sakata la mtoto Warda aliyepotea akiwa kwa mwalimu mkuu - VIDEO

FULL STORY: Sakata la mtoto Warda aliyepotea akiwa kwa mwalimu mkuu - VIDEO


Taharuki imetanda kwenye familia ya Warda Mohammed (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyumbu, Kibaha baada ya binti huyo mdogo kupotea tangu April 19, 2023.


Mama mzazi wa mwanafunzi huyo, ameeleza kuwa kama mwanaye angekuwa hai basi angemtafuta kwani huwa hawezi kabisa kukaa bila kuwasiliana naye, na kama yupo hai basi ni mgonjwa hajiwezi kitandani kwani yupo kimya sana.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kupitia kwa Kamanda wa Mkoa, RPC Pius Lutumo limetolea ufafanuzi sakata la binti mdogo, Warda Mohammed (15), mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Nyumbu, Kibaha kupotea tangu April 19, 2023.


Kamanda Lutumo amesema walipokea taarifa za kupotea kwa binti huyo kutoka kwa mtoto wa mwalimu aliyekuwa akiishi naye ambapo jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mahali alipo mwanafunzi huyo.


Kamanda Lutumo amesema matukio ya wasichana wa umri kama wa Warda kupotea, yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara na kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa zinazoweza kupatikana kwa binti huyo, aziwasilishe kwenye mamlaka yoyote anayoiamini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad