Msanii Wa Nigeria #NairaMarley Amefanya Interview Kwa Mara Kwanza Kufuatia Kifo Cha Aliyewahi Kuwa Msanii Wake Mohbad Na Kujibu Kama Anahusika Katika Namna Yoyote ile Kumuua Mohbad.
“Hapana Kwakweli, Nimekuwa Nje Ya Nigeria Tangu Agosti 1, Kingine aliondoka Kwenye Label Yangu (Marlians) Sijui Ni Lini Lakini Nakumbuka Ilikuwa 2022, Na Hatukuwahi Kumzuia Kuacha Ngoma, Kwahiyo Nilipopata Taarifa Ya Kifo Chake Nilishtushwa Sana, Nami Natakiwa Nijue Chanzo Ni Nini Kama Wengine Wanavyotaka Kufahamu, Kama Mnanilaumu Mimi, Je Nilimuua Vipi?, Sina Chakufanya kwa kifo chake, niliumizwa sana niliposikia kifo chake”
#Naira Akijibu Kuhusu Video Ya Marehemu Mohbad Aliyorekodi Akisema Kwamba Kama Akifa Basi Yeye Na Watu Wa Label Yake (Marlian) Wakamatwe
“Unajua Mi Mwenyewe Sielewi, Nilihitaji Kumpa Msaada, Halafu Kwanza Sikuwepo Kabisa Nchini (Nigeria) Wakati Anarekodi Ile Video ….”
“Mohbad alirekodi ile Video akisema Kwamba Kama Akifa Basi Mimi Na Marlians Tukamatwe!!. Na Niliporudi Nigeria Nilikutana Nae Na Kuongea Nae, Ambapo Nilimuuliza (Shida Ni Nini?) lakini Alijibu Kuwa Haelewi Chochote Na Kuniomba Msamaha” -
Lakini Pia Naira Marley Amesema Kwamba Mohbad alimuomba Msamaha Na Ushahidi Wa Mazungumzo Anao
“Nina Video Zinazoonesha Nikizungumza Na Mohbad, Wakati Nipo Marekani Mke Wake Alinipigia Simu Na Kuniambia Niongee Na Mohbad Chochote kile Kwasababu alikuwa anataka Kujiua, Kwahiyo Baada Ya Hapo Nilimpigia Na Nikawa Narekodi Mazungumzo Hayo Nikimuuliza Kwanini Anataka Ajiuwe Kwasababu Familia Yake haikuwa Sawa Kabisa (Walikuwa Stress), Nikamwambia Walau (Upate muda kidogo na Usijiue!Kwasababu ukijiua Saizi Unataka Watu Waseme Nini ?, Ikiwa Umerekodi Video Ukisema Kwamba Kama Ukifa Basi Watu Wote Wa Naira Marley Wakamatwe)
“Hivyo Kwasababu alikuwa anataka Kujiua, Nikampigia Ili Nijue Namsaidiaje, lakini alisema Kuwa mama na baba Yake Ndio Wanaelewa Shida Yake, Kwahiyo Nikamwambia Acha Nizungumze na Wazazi Wako Kama Hawatojali, Nilizungumza Nao Nikawaambia Kama Kuna Tatizo Basi akapatiwe matibabu Ila Mi sina Shida Nae Yoyote, Na Mwacheni Atulie, Asisumbuliwe na Kelele Wala Chochote kile”