Hatuna Kipa Simba, Bora Yule Dogo Salim Mara 100 Kuliko Hili Pazia l


Baada ya Simba kupata Sare ya 2 kwa 2 Dhidi ya Dynamos Ameandika Haya Gj Malisa:

Kwanza Hongereni "Uto" kwa ushindi. Pamoja na kusafiri kwa daladala za Bonyokwa lakini mmeheshimisha nchi. Kwa leo siwadai. Ningekua Rais wa nchi mngerudi kwa ndege wote kwa kazi kubwa mliyofanya. Lakini kwa kuwa sina hata udiwani, mtarudi kwa "Kosta" za Yombo viguka kama mlivyoenda. Iwe Fundisho 🤣.

Pili, Simba tumecheza "kikolo" sana leo. Baleke apewe likizo ya miezi mitatu ajifunze umaliziaji. Amepoteza nafasi nyingi za wazi. Ile nafasi ya Baleke angekua Aziz Ki, tungeondoka na magoli matano leo. Tatu; Fukuza kocha. Hatuna Kocha hapa. Kipindi cha kwanza kapanga kikosi kama anapanga chapati kwenye hotpot.

Nne; Fukuza Golikipa kwa hati ya dharura. Uto walitutania kwamba tumeleta "pazia" tukabisha,, lakini leo nasema Uto walikua sahihi. Hatuna Kipa hapa. Bora yule dogo Salim mara 100 kuliko hili pazia lililokaa golini leo. Lile goli la pili hata Joti anadaka.

Tano; Najua hapa Dar tutashinda na tutaenda Makundi, lakini lazima tukubali leo tumeaibisha taifa. Haka katimu tulikua na uwezo wa kukapiga 5 kule kwao. Sema ujinga wa Baleke, ukijumlisha na upuuzi wa Kocha, uongeze na upazia wa Kipa umetugharimu. Islamabaaaad. Bangladesh.!!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad