Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa DAR Baada ya Ajali ya Mwendokasi iliyoua Mmoja

Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa DAR Baada ya Ajali ya Mwendokasi iliyoua Mmoja


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila @albert_john_chalamila amepiga marufuku Watu wote wakiwemo Madereva bodaboda kupita barabara za mwendokasi bila ya kuwa na vibali ambapo amesema anakuja na ajenda kubwa kuhusu pikipiki zinazokatisha mwendokasi na kusababisha ajali.


RC Chalamila amesema hayo baada ya kufika kwenye mataa ya kuelekea Lumumba katikati ya kituo cha mwendokasi cha Fire na DIT Jijini Dar es salaam ilipotokea ajali ya Dereva mmoja wa bodaboda kugongwa na Basi la ‘mwendokasi’ na kupelekea kufariki papohapo.


“Basi letu zuri liendalo kwa kasi limepata ajali hapa, chanzo cha ajali Afande Muliro atatoa taarifa kwa kina lakini kwa ujumla Kijana mmoja ambaye alikuwa anaendesha pikipiki amefariki, kwenye basi bado hatujapokea taarifa kuhusu majeruhi, hii inanifundisha Mimi kama Mkuu wa Mkoa kwamba sasa kuna haja ya kuja na ajenda kubwa sana kuhusu pikipiki zinazokatisha kwenye barabara za mwendokasi, natoa rai kwa Watanzania tuache kupita barabara ya mwendokasi kama hauna kibali maalum”


Chimabe Hassan ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Bodaboda Kata ya Mwananyamala na pia ni Shuhuda wa tukio hilo ambapo amesema “Bodaboda alikuwa anatoke Fire ilikotokea mwendokasi akiwa anaelekea Lumumba, akasagwa, Bodaboda wenzangu tusipite mwendokasi ni hatari inaua, alifariki papohapo Mimi ndio nimemtoa Jamaa”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad