Kikosi Cha Simba vs Coastal union Leo September 21 NBC premier league

Kikosi Cha Simba vs Coastal union Leo September 21 NBC premier league


Ayoub
Kapombe
Hussein
Che Melone
Henock
Mzamiru
Ngoma
Chama
Baleke
Ntibazonkiza
Miquisson


Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo ambapo michezo miwili inatarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam

Wekundu wa Msimbazi Simba wanarejea katika mbio za ubingwa msimu huu wakiikaribisha Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Uhuru saa 10 jioni


Hii ni mechi muhimu kwa Simba kushinda ili kuweka morali ya wachezaji juu kuelekea mchezo wa kuwania kutinga makundi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Power Dynamos ambao utapigwa wiki ijayo

Leo mashabiki wa Simba wanatarajia 'reaction' kutoka kwa wachezaji wao baada ya mchezo dhidi ya Power Dynamos uliopigwa Zambia na kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Baada ya mazoezi ya mwisho yaliyofanyika dimba la Mo Simba Arena jana, mshambuliaji anayeongoza kwa mabao katika kikosi cha Simba Jean Baleke alitoa ahadi kuwa leo watawapa furaha mashabiki kwa kufunga mabao mengi


Ni wazi hautakuwa mchezo mwepesi kwani hata Coastal Union wamekuwa na muda mrefu wa kujiandaa na mchezo huo lakini kwa ubora wa Simba, matarajio ni kuona alama zote tatu zinabaki Msimbazi

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad