Kiwango Chambeba Morrison Kusajiliwa FAR Rabat Licha ya Mashabiki Kulalamika Utovu wa Nidhamu, Apewa Masharti Magumu



Winga mwenye vituko vingi ndani na nje ya uwanja aliyewahi kutamba nchini katika klabu za Simba na Yanga, Bernard Morrison amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuwatumikia mabingwa wa Morocco 🇲🇦 FAR Rabat, huku akitakiwa kukaa ndani ya jengo la klabu lililopo katika kambi ya jeshi.

FAR Rabat inamilikiwa na jeshi ikifundishwa na kocha wa zamani wa Yanga, Nasreddine Nabi. Licha ya winga huyo kuonyesha kiwango bora katika mazoezi ya kupima ubora wake hatua ya kumpa mkataba huo, haikuwa rahisi kutokana na rekodi mbovu juu ya nidhamu, lakini baada ya kikao kizito na mabosi wa klabu hiyo hatimaye juzi wakampa mkataba huo kuitumikia timu hiyo.

Morrison ambaye ni raia wa Ghana 🇬🇭 katika miezi hiyo 12 hatakiwi kufanya matukio yoyote ya utovu wa nidhamu na ikijitokeza mkataba wake utasitishwa mara moja na kuondoshwa klabuni. Licha ya mkataba huo mgumu, lakini Morrison katika mazoezi ya wiki mbili aliyoyafanya na FAR Rabat amewashtua kwa kiwango kikubwa, huku baadhi ya mastaa wa timu hiyo wakishinikiza asajiliwe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad