Kocha Klopp: Pesa za Waarabu ni Tishio, Hakuna TIMU Ligi ya Uingereza Inaweza Pambana Nao

 

Kocha Klopp: Pesa za Waarabu ni Tishio, Hakuna TIMU Ligi ya Uingereza Inaweza Pambana Nao

Jurgen Klopp amekiri hakuna klabu kubwa yoyote ya Ligi Kuu England yenye nguvu ya kushindana na mkwanja mrefu wa usajili wa Saudi Arabia huku kocha huyo wa Liverpool akipambana kumbakiza winga wake, Mohamed Salah.


Al-Ittihad ya Saudi Arabia iliwasilisha ofa yake ya pili ya Pauni 170 milioni (Sh 538bilioni), kwa ajili ya kumsajili Mo Salah usiku wa juzi, saa kadhaa baada ya Liverpool kukataa ofa ya awali ya Pauni 150 milioni.


Liverpool inapambana na inasema Mo Salah atabaki Anfield, lakini klabu hiyo ya Saudi Pro League ipo tayari kuongeza pesa na kumsajili mchezaji huyo kwa ada itakayoweka rekodi ya dunia ya Pauni 200 milioni.


Dirisha la usajili huko England limefungwa, lakini mabosi wa Anfield kijasho kinawatoka kwelikweli kwa sababu klabu za Saudi Pro League zitaendelea kufanya usajili hadi Alhamisi ijayo.


Klopp alisema: “Wiki ijayo tunajua ni changamoto kiasi gani tutakayokuwa tumekabiliana nayo. Naona kama hii imekuwa tishio kubwa. Sioni unawezaje kukataa. Tufanye nini? Mikataba ni ya pesa nyingi sana, inasababisha matatizo makubwa. Hakika.


“Tunapaswa kuhakikisha ligi za Ulaya zinaendelea kubaki na nguvu kama vinavyopaswa kuwa. Pengine tubadilishe sheria na taratibu, sivyo? Sote tunashangazwa na shughuli zinazoendelea. Wachezaji wengi sana wameenda.”


Ripoti zinadai kwamba, Mo Salah, 31, amepewa ofa ya kulipwa mshahara wa Pauni 2.3 milioni kwa wiki wakati atakapotua huko Mashariki ya Kati.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad