KOCHA Robertinho: Muda Ukifika Mtaziba Midomo yenu Kuhusu Simba

 


Wakati Droo kwa ajili ya mashindano ya Afrika Super League inatarajia kufanyika leo Jumamosi (Septemba 02) majira ya usiku, Kocha Mkuu wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ ametambulisha mbinu mpya kwa wachezaji wake za kuhakikisha wanatumia vyema mipira ya krosi ili kufunga mabao kwenye michezo mbalimbali wanayocheza.


Kwa sasa Simba SC inajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa Mzunguumo wa pili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaochezwa Septemba 16, mwaka huu kwenye Uwanja wa Levy Mwanawasa ulioko katika mji wa Ndola, Zambia.


Simba SC ambayo imeanza msimu huu kwa kubeba Ngao ya Jamii mbele ya watani zao Young Africans, itachuana katika kuwania taji la Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mashindano ya Kombe la FA.


Katika mazoezi ya kikosi cha Simba SC yanayoendelea Uwanja wa Mo Simba Arena, imeshuhudiwa Robertinho akiwataka wachezaji warudie mara kwa mara zoezi hilo ambalo anaamini likifanikiwa, litasaidia katika kuongeza nguvu na hatimaye timu kufikia malengo.


Kocha huyo amesema timu yake inaendelea kuimarika siku hadi siku licha ya baadhi ya wachezaji wachache bado hawajafikia ubora anaouhitaji lakini anaamini kabla ya kukutana na Power Dynamos watakuwa wamneimarika.


Mbrazil huyo alitumia saa mbili kwa ajili ya kukiona kikosi cha timu hiyo kwa kufanyia pia kazi mipira ya faulo na alifurahishwa kuona makipa wake, Ally Salim na Hussein Abel, wakiwa makini kudaka mipira kwenye zoezi hilo.


Pia, imeshuhudiwa kipa chaguo la kwanza la timu hiyo, Aishi Manula akianza programnu maalum ya mazoezi kwa ajili ya kurejea langoni. Manula alikuwa akifanya mazoezi binafsi chini ya uangalizi wa daktari wa timu hiyo, Edwin Kagabo.


Baada ya mazoezi kumalizika, Robertinho alisema licha ya safu yake ya ushambuliaji kuendelea kufunga katika kila mchezo, bado anawataka kuona wanaongeza bidii ya kuwa makini.


“Mipango yetu ipo katika michuano iliyopo mbele yetu, tunaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika licha ya kuwakosa baadhi ya wachezaji ambao wamekwenda katika timu zao za taifa lakini hatuwezi kukaa bila ya kujiimarisha.


“Kikubwa tupo katika wakati mzuri kwa sababu timu inapata matokeo ya ushindi wakati wote na inatengeneza nafasi, ingawa nataka kuona wakitumia vyema mipira ya krosi kufunga mabao ambayo yatatusaidia kupiga hatua kubwa na kupunguza presha ambayo itakuwa kwenye upande wetu,” amesema Robertinho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad