"Nimejenga mazingira ya kuwa na timu iliyo na uwiano mzuri kwa kila idara, tazama tumefunga magoli mengi lakini vile vile tumeruhusu goli moja tu katika michezo saba tena bao la penati ambalo ilikuwa kosa letu. Sasa ili uwe na uwiano na namna hiyo lazima ujenge timu inayotegemeana na sio timu inayomtegemea mtu fulani kwenye idara fulani.
"Jambo ambalo nimezingatia kwanza ni wachezaji kuheshimiana wenyewe kwa wenyewe, pili wachezaji kuheshimu falsafa zangu, huwezi kuwa kocha mzuri kama wachezaji hawakuheshimu. Kimsingi matokeo chanya ya sasa ni kutokana na jitihada za wachezaji na benchi la ufundi.
Amesema Kocha wa Klabu ya Yanga miguelgamondi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari.