Kolabo Moja na Diamond Platnumz ni Tsh Milioni 120 - Baba Levo Afichua

 

Kolabo Moja na Diamond Platnumz ni Tsh Milioni 120 - Baba Levo Afichua

Unaambiwa kazi sio kumpata supastaa wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz ili kufanya naye kolabo, kazi ni kuzipata hizo pesa anazotaka ili uweze kumlipa afanye na wewe ngoma moja.


Hilo ametueleza msanii Baba Levo kupitia video hii akiwa na Billsepenga akifunguka kuwa Diamond Platnumz anatoza Tsh Milioni 120 kufanya Collabo 1.


Baba Levo akizungumzia suala hilo; "Kolabo na Diamond ni tsh milioni 120, kwa hiyo ni kazi kwelikweli, sio kazi kumpata kazi ni kuzipata hizo hela. Ukimlipa anafanya.


"Mimi siwezi kumlipa kwa sababu niko naye kila muda na mimi sasa hivi sio chawa ni kupe. Sisi ni wasanii wazee, ukipata ka-hit kamoja aunamshukuru Mungu.


"Zuchu amekuwa akinipandikizia nyimbo zangu, nikiachia naye anaachia, sasa ntamfanyaje na ni shemeji yangu, nimejaribu kwenda kumsema kwa Diamond lakini Diamond anamsikiliza Zuchu kuliko mimi, nikasema mambo ya mapenzi haya," amesema Baba Levo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad