Kumekucha...Mke wa Bilionea Msuya akutwa na kesi ya kujibu



MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imemkuta na kesi ya kujibu aliyekuwa mke wa mfanyabiashara wa madini mkoani Arusha, marehemu Erasto Msuya maarufu kwa jina la Bilionea Msuya, Miriam Mrita anayetuhumiwa kumuua wifi yake Aneth.

Mbali na Mrita mshtakiwa mwingine aliyekutwa na kesi hiyo ya kujibu ni mfanyabiashara Revocatus Muyela, ambao wamedai kuwa wataleta mashahidi na vielelezo kuthibitisha tuhuma hizo dhidi yao na pia watajitetea kwa kiapo.

Uamuzi huo mdogo ulitolewa na Jaji Edwin Kakolaki wa mahakama hiyo, baada ya upande wa mashitaka kufunga kesi yao kwa mashahidi 25 na vielelezo mbalimbali kikiwemo kisu ambacho kinadaiwa kilitumika kumchinja koromeo.

Jaji Kakolaki alisema mahakama baada ya kuzingatia ushahidi na vielelezo vilivyotolewa, mahakama imejiridhisha kwamba kuna kesi ya msingi ambayo inawatosheleza washitakiwa wajitetee kama sheria inavyoelekeza.


“Washitakiwa simameni, kwa mujibu wa kifungu 293 (2) na (a) (b) na Cha (3) inawafahamisha pamoja na haki zenu nilizokwisha waeleza na pia mawakili wenu watawaelewesha kama mtakuwa hamjaelewa vizuri,”

“Mnaweza kutoa ushahidi nyie wenyewe au kuita mashahidi, ambapo mashahidi wenu wataulizwa maswali kama walivyokuwa wanaulizwa hawa wengine, pia kuna haki ya kukaa kimya, wakati unatumia haki hii mahakama kuchukulia vinginevyo ambavyo itaona inafaa na kuendelea kutoa uamuzi,” alisema Jaji Kakolaki

Pia, Jaji Kakolaki alisema kuwa kujitetea kwao wanaweza kujitetea kwa kiapo, haya washitakiwa mnaweza kuzungumza na mawakili wenu.


Washitakiwa hao walizungumza na mawakili wao Peter Kibatala na Nehemiah Nkoko, ambapo walifia hatua ya kuieleza mahakama hatua ambazo watazitumia.

Mshitakiwa wa kwanza, Mrita aliieleza mahakama kuwa atajitetea kwa kiapo na atakuwa na mashahidi wa kumtetea pamoja na vielelezo, ambapo kwa juzi hakuweza kusema idadi akaomba muda kidogo wa kufanya maandalizi.

Kwa upande wake, Muyela alidai kuwa ushahidi wake atautoa kwa kiapo na pia atakuwa na mashahidi na vielelezo.

“Baada ya kusikia hatua zenu na pia kwa kuzingatia muda wa kiko hiki cha mahakama umefikia kiko, hatuwezi kuendelea hadi pale msajili wa Mahakama Kuu atakapopanga kikao kingine, kwa hiyo mtajulishwa,” alisema Jaji Kakolaki


“Niwashukuru pande zote mbili, watumishi wa mahakama, waandishi wa habari na ndugu na jamaa kwa kuweza kuwa na utulivu na kumaliza kiko hiki kwa usalama,” alisema

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Paul Kimweri alidai kuwa Getruda Mfuru ndiyo shahidi wao wa mwisho hawataleta shahidi mwingine.

“Tunaiyachia mahakama itafakari kama washitakiwa wanakesi ya kujibu au la,”alidai Kimweri

Kwa upande wa Kibatala na Nkoko alidai kuwa hawana pingamizi lolote na wanasubiri uamuzi wowote wa mahakama wataupokea.


Miriam ambaye ni mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji hayo ya wifi yake huyo Aneth aliyeuawa Mei 25, 2016 kwa kuchinjwa shingoni nyumbani kwake, Kibada Kigamboni , jijini Dar es Salaam, amekiri kuhusika na mauaji hayo, katika maelezo yake ya onyo.
[18/09, 19:31] Janeth Jovin: Watumishi 7 halmashauri ya Liwale kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Mohamed Mchengerwa amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo kuwachukuli hatua za kinidhamu watumishi saba wa halmashauri ya Liwale mkoani Lindi kwa kushìndwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Watumishi hao wameshinda kutekeleza majukumu hayo hivyo kuzorotesha utendaji kazi wa shughuli mbalimbali za halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali cha wizara hiyo, Nteghenjwa Hosseah amewataja watumishi hao ni Kaimu Mhandisi wa Wilaya Sisty Njau, Mkuu wa Idara ya Maliasili Damasi Mumwi, Mkuu wa Idara ya Kilimo na Ushirika Mustafa Magembe.

Wengine ni Mkuu wa Idarà ya Ugavi na Ununuzi Vinsenti Moyo, Mkuu wa Idara ya Tehama Mohamed Songolo, Katibu wa Afya Sadick Khatibu pamoja na Ofisa Ugavi na Ununuzi aliyehamishiwa halmashauri ya Wilaya ya Kilwa Tunu Mtamaha

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad