Kwa Maandalizi Haya Power Dynamo Wakipona Mbele ya SIMBA Niko Pale Nimekaa Mniite Kuku

 

Kwa Maandalizi Haya Power Dynamo Wakipona Mbele ya SIMBA Niko Pale Nimekaa Mniite Kuku

Kwa Maandalizi Haya Power Dynamo Wakipona Mbele ya SIMBA Niko Pale Nimekaa Mniite Kuku

UONGOZI wa Simba, umeweka wazi kuwa, muda uliopo kwa sasa ni benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kusuka silaha za maangamizi kwenye mashindano ya kimataifa.

Timu hiyo ina pointi sita kibindoni baada ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu Bara, huku safu yake ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao sita na ile ya ulinzi imeruhusu mawili.

Mchezo wao ujao kimataifa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos unaotarajiwa kuchezwa Septemba 16, mwaka huu Uwanja Levy Mwanawasa, Zambia.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, alisema: “Silaha za ushindi kwenye mechi za kimataifa lazima ziandaliwe vizuri, unajua kwamba ili kupata ushindi lazima wachezaji wawe tayari na hilo wanalitambua, hatuna mashaka.

“Kila kitu tunaamini kitakuwa sawa, wapinzani wetu tunatambua wanajua wanakutana na timu ya aina gani. Inapofikia hatua ya mechi za kimataifa hilo ni suala kubwa na tunawaheshimu wapinzani wetu ila ambacho tunafanya ni kuwa tayari.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad