Mahakama Kuanza Kusikiliza Ushahidi Kesi ya Aliyemuua Mkewe na Kumchoma Moto

 

Mahakama Kuanza Kusikiliza Ushahidi Kesi ya Aliyemuua Mkewe na Kumchoma Moto

Mahakama Kuu ya Tanzania, inatarajia kusikiliza mashahidi 28 pamoja na vielelezo 15 katika kesi ya mauaji inayomkabili Hamis Luoga, anayekabiliwa na shtaka la kumuua mkewe Naomi Marijani.


Luoga anadaiwa kumuua mkewe Naomi kisha kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na baadaye kuyachukua majivu ya marehemu na kwenda kuyafukia shambani kwake.


Wakili wa Serikali, Dorothy Massage, amezungunza hayo leo Septemba 6, 2023; shauri hilo lilipokuja kwa ajili ya kumsomea mshtakiwa huyo hoja za awali. "Jumla tuna mashahidi 28 na vielelezo 15 ambavyo tunatarajia kutumia katika ushahidi wa upande wa mashtaka," amedai Massawe.


Akisoma hoja za awali Wakili Massawe amedai kuwa Mei 15, 2019; maeneo ya Gezaulole, wilayani Kigamboni, mshtakiwa huyo alimuua kwa makusudi mkewe Naomi.


Inadaiwa mshtakiwa huyo aliripoti katika kituo cha polisi cha mji Mwema kuwa mkewe Naomi pamoja na mwanaye wametoweka tangu Julai 27, 2019.


Inadaiwa alipoenda kituoni hapo, na kuhojiwa na polisi mshtakiwa huyo alikiri kumshambulia mkewe hadi kufa na kisha alichukua mwili wa Naomi na kupeleka kwenye kibanda na kuuchoma kwa mkaa.


Inadaiwa kuwa baada ya kuuchoma mwili huo aliuchukua mabaki ya majivu ya mkewe kisha kuyaweka kwenye mfuko na kwa kutumia kutumia gari lake aina Subaru Forester, alikwenda kuyafukia shambani kwake eneo la Mlogolo, wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.


Massawe alidai kuwa katika mahojiano hayo mshtakiwa anadai kuwa alichimba shimo kwenye shamba lake Kisha kuweka hayo majivu akayafukia na kupanda mgomba juu yake.


Baada ya maelezo ilichukuliwa vinasaba vya majivu ya marehemu kwenda kupima kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ambapo ilibainika kuwa aliyefariki alikuwa Naomi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad