Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekataa pingamizi la Mbunge wa zamani, Vicky Kamata la kupinga uteuzi wa mtoto wa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Servacius Likwelile kuwa msimamizi wa mirathi na mali za marehemu zenye thamani ya zaidi ya Tsh. Bilioni 4
Mahakama imeeleza Dkt. Likwelile alifunga Ndoa na Mary Ibrahim katika Kanisa Katoliki Mwaka 1994 na kwa mujibu wa Sheria ya Ndoa Tanzania Sura ya 29 kifungu 10 (a) na (b) kama ilivyofanyiwa marejeo na Bunge Mwaka 2019 ilikuwa ni ya mke mmoja, hivyo ndoa ile iliyofungwa Machi 19, 2016 haikuwa halali na hakukuwa na uthibitisho wa kuvunjika kwa Ndoa ya awali
Jaji ameamua kuwa mali ambazo Vicky alipinga kuingizwa katika orodha ya mali za marehemu Dkt. Likwelile (aliyefariki Februari 19, 2021) akidai ziliingizwa kimakosa, zijumuishwe katika orodha ya mali za marehemu
Kwa tafsiri ya Mahakama, Masuria ni Wenza wanaoishi pamoja bila Ndoa halali, hivyo Vicky Kamata anakosa uhalali wa kuwa sehemu ya Warithi wa Mali.