Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu Yaiamuru Tanzania Kufuta Hukumu ya Viboko



Mahakama ya AfCHPR imeeleza kuwa Tanzania inapaswa kufuata Mabakubaliano ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu kwa kuondoa Adhabu za Utesaji, Ukatili, Unyama na Udhalilishaji

Pia, Jopo la Majaji 11 limeagiza Mamlaka za Tanzania kuwasilisha Ripoti kuhusu utekelezaji wa amri hiyo kila baada ya miezi 6 hadi pale Mahakama itakaporidhishwa na utekelezaji kamili wa katazo hilo

Majaji waliokaa Jijini Arusha ili kupitia Rufaa ya Mtanzania Yassin Rashid Maige aliyehukumiwa mwaka 2003 kutumikia Kifungo cha Miaka 30 na Viboko 12 kwa Wizi wa kutumia Silaha, waliamua kuwa Mahakama za Tanzania zilikiuka Haki ya Utu ya Maige kwa kuamuru achapwe Viboko 12 kama sehemu ya adhabu yake

Ikumbukwe, Rufaa ya Maige ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu hivyo aliamua kuwasilisha ombi lake katika Mahakama ya Afrika (AfCHPR) Juni 2017 ambapo Mahakama hiyo imezitaka Mamlaka za Tanzania kumlipa Maige Tsh. 300,000 kama Fidia ya kuchapwa Viboko

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad