Mama mzani wa kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki raia wa Burkina Faso amefunguka kuwa vilabu viwili Tanzania ambavyo ni Simba na Yanga vilikuwa vikiwania saini ya mwanaye wakati wa dirisha kubwa la usajili 2022/23.
Lakini Aziz Ki alipokuja Tanzania kucheza na Simba wakati akiwa na Asec Mimosas kwenye Kombe la Shirikisho Afrika (2021/22) hakupenda namna ambavyo Simba wanacheza hivyo akaanza kuangalia aina ya uchezaji wa Yanga na akaupenda hivyo akaamua kuichagua Yanga japo ofa yao haikuwa bora kushinda timu nyingine zilizomfuata ila alichagua sehemu ambayo anaweza kukua.
"Baada ya kucheza kwa mafanikio makubwa kwa miaka miwili pale ASEC Mimosas, kuna vilabu vinne vilileta ofa ya kumtaka Aziz, moja kutoka Misri, moja kutoka Morocco na nyingine mbili kutoka Tanzania.
"Yeye alitamani akacheze Misri ili aonekane na baadae aende Qatar kwani ndiyo ilikuwa ndoto yake akijua atapata pesa. Alisema anacheza mpira sawa lakini mkononi hana kitu, anataka acheze mpira apate pesa.
"Eng. Hersi Said alisafiri mpaka Morocco kuonana na Aziz wakazungumza kuhusu uwezekano wa kumsajili lakini asingeweza kusaini mkataba. Alirudi tulishauriana tukashirikisha ma watu wengine wakashauri kule Uarabuni kuna ubaguzi mkubwa, leo atapangwa kesho hatacheza na kipaji chake kitakufa, hivyo tukawa tumepiga chini ofa ya Misri na Morocco ikabaki Simba na Yanga.
"Aziz alisema amecheza na Simba Sc alipokuja Tanzania akiwa na ASEC Mimosas lakini hakupenda aina ya uchezaji wao, hivyo akaanza kufuatilia Yanga akaona wanacheza vizuri akavutiwa na staili yao ya uchezaji na mbinu zao uwanjani, mwisho wa siku akachagua Yanga.
"Hakuchagua Yanga kwa sababu ya pesa, kwa sababu amgetaka pesa angeenda Misri au Morocco ambao walikuwa na ofa kubwa kuliko ya Yanga, alichagua Yanga ili kukuza kipaji chake na kuonekana zaidi," amesema Mama wa Aziz Ki.