Mbowe alaani ukamatwaji wa Lissu, “Tuna hofu kubwa”





MWENYEKITI wa Chadema, Freema Mbowe amelaa ukamataji, unyanyasaji, usumbufu aliodai unafanywa  na Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya Dola kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa aliyoweka kwenye ukurasa wake wa Twitter, Mbowe amesema Chadema kinalaani ukamati huo pia kwa viongozi wengine waandamizi wa ngazi mbalimbali, wanachama na wapenzi wa chama hicho mkoani Arusha.

“Kwa uzito huo huo, tunalaani uzuiaji wa mikutano yetu na shughuli halali za kisiasa huko Ngorongoro, Loliondo na Karatu.

“Tuna hofu kubwa ya usalama wa watu wetu na ni dhahiri sasa Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan inarejesha utawala wa mabavu usiothamini haki, Uhuru na Demokrasia. Tunafuatilia kwa karibu na tunadai kuachiliwa haraka na bila masharti kwa watu wetu wote!,” ameandika Mbowe.


Taarifa hiyo ya Mbowe imekuja saa chache baada ya Jeshi la Polisi mkoani Arusha kukiri kumkamata Lissu na wenzie watatu kwa ajili ya mahojiano kuhusu tuhuma za kufanyq mikusanyiko isivyo halali na kuzuia Polisi kutekeleza majukumu yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad