McDonald's Yashitakiwa kwa Kumpa Mteja Kahawa ya Moto kupita kiasi

 

McDonald's Yashitakiwa kwa Kumpa Mteja Kahawa ya Moto kupita kiasi

Mgahawa maarufu Duniani McDonald’s Mjini San Franscisco imeshutumiwa kwa kutoa kikombe cha kahawa kilichokuwa cha moto kupita kiasi huku mbaya zaidi kikombe kicho kilikuwa hakijafungwa vizuri, ikipelekea kahawa hiyo kumwagika kwenye mwili wa Mable Childress na kusababisha majeraha kinywani mwake.


Kesi hiyo iliyowasilishwa wiki iliyopita, ilidai kwamba Mwanamke huyo alipata maumivu makali ya kimwili na kihisia ambapo uzembe wa mgahawa huo ulikuwa sababu kubwa kwa majeraha yake.


Childress pia amesema katika kesi hiyo Wafanyakazi wa Mc Donald walikataa kumsaidia, jambo ambalo McDonald's walikanusha “Tunachukua kila malalamiko ya Wateja kwa uzito na wakati Childress, Wafanyakazi wetu na Timu ya usimamizi ilizungumza nae ndani ya dakika chache na kutoa msaada”


Kesi hii inalingana na kesi maarufu ya kahawa ya McDonald miongo kadhaa iliyopita, ambapo Mwanamke mwingine alimwaga kahawa kwenye mapaja yake na kuchomwa na kupata majeraha, Mlalamikaji katika kesi hiyo alilipwa karibu dola milioni 3 (Tsh bil 7.5) na kisha akalipwa $480,000 (Tsh Bil 1.2) baada ya kampuni hiyo kukata rufaa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad