Erling Haaland |
Mabingwa watetezi, Manchester City wameendeleza ubabe katika Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua Fulham mabao 5-1 Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Ilikuwa siku kwa mshambuliaji Mnorway, Erling Haaland aliyepiga hat-trick kwa mabao yake ya dakika za 58, 70 kwa penalti na 90 na ushei kufuatia Julian Alvarez kufunga la kwanza dakika ya 31 na Nathan Ake kufunga la pili dakika ya 45 na ushei.
Bao pekee la Fulham limefungwa na Tim Ream dakika ya 33, matokeo ambayo yanawafanya wabaki na pointi zao nne za mechi nne, wakati ushindi wa leo ambao ni wa nne mfululizo unaifanya Man City ifikishe pointi 12 na kuendelea kuongoza Ligi.